Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) imepongeza kurushwa kwa satelaiti tatu zilizotengenezwa zilizotengenezwa na wataalamu wa hapa nchini, na kuitaja hatua hiyo kuwa mafanikio ya kihistoria katika mpango wa anga za mbali wa Jamhuri ya Kiislamu.

Katika kikao cha wazi cha Bunge la Iran leo Jumatano, wabunge 190 walitia saini taarifa ya kuipongeza Wizara ya Habari na Teknolojia ya Mawasiliano na wanasayansi wa anga za juu wa Iran kwa kurusha kwa wakati mmoja satelaiti tatu zilizotengenezwa hapa nchini.

Wametunga sheria hao wa Iran wametaja mafanikio hayo kuwa hatua muhimu ya kihistoria kwa teknolojia ya anga za juu ambayo inasisitiza kukua kwa Iran kiteknolojia, kujitegemea na kupanua uwepo wake katika medani ya anga ya kimataifa.

Jumapili ya Disemba 28, Iran ilirusha hadi kwenye obiti, satelaiti tatu zilizobuniwa na kutengenezwa ndani ya Iran. Hii ni mara ya kwanza kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kurusha satelaiti nyingi angani kwa wakati mmoja. Iran hivi sasa imejiunga na klabu ya takriban nchi 10 duniani ambazo zina uwezo wa kubuni, kutengeneza na kurusha satelaiti katika anga za mbali.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Iran ametangaza kwamba mawimbi ya kwanza ya satelaiti zote tatu zilizobuniwa na kutengenezwa ndani ya Iran zinazoitwa “Zafar 2”, “Paya” na “Kowsar” zilizotumwa angani Jumapili jioni, yamepokewa kwa mafanikio ardhini akisisitiza kuwa, hii inathibitisha uzima wa kiufundi na utendajikazi mzuri wa satelaiti hizo za Iran baada ya kuingia kwenye mzingo (obiti).

Kwa mujibu wa shirika la habari la Press TV, mara hii Iran ilitumia kituo cha kurushia satelaiti cha Vostoch-ny Cosmod-rome cha Russia kurusha satelaiti zake hizo ambazo ni za teknolojia ya kisasa zaidi. 

“Hatua hii ya kimkakati na muhimu sio tu mafanikio makubwa ya kiufundi, lakini pia ni hatua ya mabadiliko katika historia ya teknolojia ya anga ya nchi hii,” imesema taarifa ya Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) wa Iran, Sattar Hashemi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *