“Mimi ni Mjasiriamali nilianza kwa kuajiriwa . Nilifika Dubai 2019. Nilikwenda kwa lengo la kutafuta ajira baada ya kuhitimu masomo yangu.
“Kabla ya kwenda Dubai nilikwenda South Africa lakini sikufanikiwa nilichokitaka. Niliangalia upande mwingine. Niliona sehemu nyingine ya kwenda kutafuta ajira ni Dubai.
“Sikuanza na mtaji mkubwa sana. Nilianza kwa kuajiriwa. Wakati nafanya kazi pale nilikuwa najifunza kwenye shughuli zangu nilizokuwa nafanya pale na pia kwenye shughuli zingine ambazo ningezifanya kwa baadae.
“Na kujifunza kwangu nilipata fursa ya kujuana na watu mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali. Nilipotoka kwenye kujifunza nilikwenda kwenye kujaribu kuanza biashara yangu mwenyewe ili niweze kutimiza malengo yangu makubwa ambayo nilikuwa nimejiwekea mbeleni”- Hussein Jamal, Mjasiriamali.
#LiveonClouds360
#Clouds26Nyoosha
#LainiYawana