Mali na Burkina Faso zinasema zitawazuia raia wa Marekani kuingia katika nchi zao, katika kile wanachoeleza kuwa ni jibu la moja kwa moja kwa uamuzi wa Washington wa kuwazuia raia wao Marekani.

Mataifa hayo mawili ya Afrika Magharibi yanayoongozwa na kijeshi yalitangaza hatua hiyo Jumanne usiku, yakisema hatua hiyo inaanza mara moja.

Uamuzi huo unafuatia vikwazo vya usafiri vya Marekani vinaloathiri mataifa kadhaa barani Afrika na Mashariki ya Kati, vililoamriwa na Rais Donald Trump.

Wizara ya mambo ya nje ya Mali ilisema inatekeleza kanuni ya usawa, na kuongeza kuwa raia wa Marekani sasa watakabiliwa na masharti yale yale ya kuingia nchini Mali yaliyowekwa na Marekani.

Serikali ya Burkina Faso imesema itaendelea kujitolea kudumisha usawa wa uhuru, na kwamba bado iko wazi kwa ushirikiano na washirika wa kimataifa ambapo maslahi yanalingana.

Mali na Burkina Faso, pamoja na nchi jirani ya Niger, hivi majuzi zilijiondoa katika jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi Ecowas na kuunda Muungano wa Mataifa ya Sahel.

Mataifa hayo yamejitenga na washirika wa Magharibi na kuimarisha uhusiano na Urusi.

Nchi nyingine za Kiafrika zilizoathiriwa na marufuku iliyopanuliwa ya hivi karibuni ya Marekani, ikiwa ni pamoja na Nigeria na Sierra Leone, zimesema zinapanga kujibu kupitia njia za kidiplomasia.

Hatua za Marekani zinapaswa kuanza kutumika tarehe 1 Januari 2026.

Mapema mwaka huu, Chad pia ilichukua hatua ya kulipiza kisasi baada ya kujumuishwa katika awamu ya kwanza ya vikwazo, kusitisha utoaji wa viza kwa raia wa Marekani.

Rais Mahamat Idriss Déby Itno alisema hatua hiyo inahusu utu wa taifa, akiongeza kuwa Chad inaweza kukosa utajiri au ushawishi, lakini haitakubali kudhulumiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *