
Wakili maarufu wa Uganda na mwanaharakati wa haki za binadamu, Sarah Bireete, amekamatwa na polisi wa Uganda, shirika lisilo la kiserikali analoliongoza limeshutumiwa mnamo Desemba 30, 2025. Kipindi hiki cha hivi karibuni cha ukandamizaji kinakuja wakati uchaguzi wa urais na wa wabunge uliopangwa kufanyika mwezi Januari.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakili nchini Uganda na mtetezi wa haki za binadamu Sarah Bireete alikamatwa Jumanne huko Kampala, mji mkuu wa Uganda. Msemaji wa polisi alithibitisha kukamatwa kwake jioni ya Jumanne, lakini sababu ya kukamatwa kwake bado haijulikani. Kukamatwa huku kumezua wasiwasi miongoni mwa watetezi wa haki za binadamu wakati uchaguzi wa rais unakaribia.
Alizuiliwa nyumbani kwake. Dakika chache mapema, alichapisha tahadhari kwenye mitandao ya kijamii. “Nyumba yangu imezingirwa na polisi na jeshi,” aliandika. Jioni, polisi wa Uganda walithibitisha kuzuiliwa kwake, lakini bila kutaja sababu au kutangaza mashtaka yoyote yanayomkabili. Kulingana na msemaji wa polisi wa Uganda, Sarah Bireete atafikishwa mahakamani “kwa wakati unaofaa,” mara tu uchunguzi utakapokamilika. “Uchunguzi unaendelea,” alielezea.
Kiongozi mwenye msimamo wa wastani
Sarah Bireete anaongoza Kituo cha Utawala wa Katiba. Akiwa wakili anayeheshimika, alikuwa mtoa maoni wa kawaida katika vyombo vya habari na alijitambulisha kama sauti ya kukosoa masuala ya utawala na utawala wa sheria. Katika wiki za hivi karibuni, alikuwa akishiriki baadhi ya mada za kampeni za kiongozi wa upinzani Bobi Wine kwenye mitandao ya kijamii. Lakini bado anachukuliwa kuwa kiongozi mweye msimamo wa wastani.
“Polisi wa Uganda wamethibitisha kukamatwa kwa mkurugenzi wetu mkuu, Sarah Bireete. Walisema kwamba kwa sasa yuko kizuizini na atafikishwa mahakamani kwa wakati unaofaa.”
Kukamatwa kwake, wiki mbili kabla ya uchaguzi wa urais, kunachochea hofu ya hali ngumu ya kisiasa, huku Rais Yoweri Museveni akitafuta muhula mwingine baada ya karibu miaka 40 madarakani.
Watu kadhaa wa mahirika ya kiraia wanalaani ukosefu wa maelezo na kudai uwazi zaidi kuhusu kukamatwa kwake.