Serikali ya Kenya imeliandikia rasmi barua shirikisho la soka la Afrika CAF, liruhusu mashabiki wa Kenya kuujaza uwanja wa Kasarani, wakati wa mchezo wa robo fainali dhidi ya Madagascar, unaotarajiwa kufanyika Ijumaa ya wiki hii.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Jumatano ya wiki hii Waziri wa michezo wa Kenya, Salim Mvurya, alisema shirikisho la soka FKF pamoja na kamati ya maandalizi ya CHAN, waliiomba CAF kuruhusu mashabiki elfu 48 kuingia kwenye uwanja huo.

CAF iliagiza mecho zilizosalia za Harambee stars kushuhudiwa na mashabiki elfu 27 pekee baada kujirudia kwa matukio ya utovu wa usalama yaliyosababishwa na mashabiki kulazimisha kungia uwanjani katika mechi za awali za hatua ya makundi.

Kenya itacheza dhidi ya Madagascar katika mechi ya robo fainali katika uwanja wa Kasarani.
Kenya itacheza dhidi ya Madagascar katika mechi ya robo fainali katika uwanja wa Kasarani. © PsymonSays

Kenya pia ilipigwa faini ya shilingi za kenya milioni 12 kutokana na vitendo hivyo vilivyoshuhudiwa kwenye mechi za Morocco, Angola na DRC, CAF pia ikionya kuwa itahamisha mechi za Harambee star kwenye uwanja mwingine ikiwa matukio ya kiusalama yatajirudia.

Haya yanajiri wakati huu haifahamiki hadi sasa ni mashabiki wangapi walifanikiwa kununua tiketi mtandaoni, baada ya kampuni iliyopewa zabuni ya Mookh Africa kutangaza kusitisha zoezi la uuzaji siku ya Jumanne kufuatia tovuti yake kudukuliwa, kwa sasa tovuti ya tiketi ikionesha tiketi zote zimenunuliwa.

Mashabiki walijaa uwanjani Kasarani kupita kiasi wakati wa mechi ya Kenya na Morocco
Mashabiki walijaa uwanjani Kasarani kupita kiasi wakati wa mechi ya Kenya na Morocco © CAFOnline

Katika hatua nyingine, kamati ya maandalizi ya CHAN ya Uganda, hapo jana imetangaza marufuku kwa mashabiki kuvaa jezi au mavazi yaliyoandikwa matamshi yenye ukakasi na kukosa maadili, tangazo linalotolewa baada ya picha zilizosambaa mtandaoni zikionesha baadhi ya mashabiki wakiwa wamevaa tisheti au jezi za timu ya taifa ya Uganda zenye maandishi ya matusi na kufedhehesha.

Ikumbukwe kuwa katika mashindano ya mwaka huu, vitu kadhaa vilipigwa marufuku uwanjani ikiwemo filimbi, vuvuzela na ngoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *