Taulo za Softcare zazua hofu na maswali Senegal
Tuhuma dhidi ya kampuni ya Softcare kuhusu matumizi ya malighafi zilizokwisha muda zimeibua hasira Senegal, zikichochea uchunguzi, maandamano na hofu ya usalama wa taulo za kike.
Tuhuma dhidi ya kampuni ya Softcare kuhusu matumizi ya malighafi zilizokwisha muda zimeibua hasira Senegal, zikichochea uchunguzi, maandamano na hofu ya usalama wa taulo za kike.
Wapatanishi wa Ukraine na Urusi wameanza duru ya pili ya mazungumzo yanayosimamiwa na Marekani Jumatano huko Abu Dhabi, wakiendeleza juhudi za kumaliza mzozo mkubwa zaidi barani Ulaya tangu Vita vya…
Ukraine imesema imeridhishwa na jinsi mazungumzo kuhusu vita kati yake na Urusi yanavyokwenda huko Abu Dhabi. Mazungumzo hayo yaliyoanza jana yanaendelea tena leo huku Ukraine ikipania kusisitiza dhamana ya usalama.
Iran na Marekani zitafanya mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran nchini Oman siku ya Ijumaa. Mazungumzoi hayo yalikuwa yafanyike nchini Uturuki.
Kundi la waasi wa M23 limedai kuhusika na shambulizi la ndege zisizo na rubani lililolenga uwanja wa ndege muhimu mjini Kisangani kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekutana na mwenzake wa Misri Abdel Fattah al-Sisi mjini Cairo Jumatano. Ametia saini mikataba mipya ya ushirikiano na kuashiria umoja wa pande mbili kuhusu…
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ameanza ziara yake ya kwanza ya eneo la Ghuba itakayompeleka Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Iran na Marekani zimekubaliana kufanya mazungumzo ya nyuklia kesho Ijumaa nchini Oman+++Hasira na maswali mengi yanaendelea kuibuka nchini Senegal, kufuatia tuhuma nzito dhidi ya kampuni ya Kichina ya Softcare, inayotengeneza…
Ukraine yasema mazungumzo na Urusi na Marekani yanayoendelea Abu Dhabi ni ya tija. Iran na Marekani kufanya mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia nchini Oman. Na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz…
Baada ya mkasa wa mgodi wa madini ya coltan mjini Rubaya, mashariki mwa Kongo mamia ya familia ziko na sintofahamu. Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 200 wamefariki. Je nani anawajibika…
Chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar cha ACT-Wazalendo kimepinga mpango wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, ZEC wa kuteketeza nyaraka zote za uchaguzi mkuu uliofanyika October 29, 2025 na kusema…
Serikali ya Rais Donald Trump inapunguza idadi ya maafisa wa uhamiaji huko Minnesota baada ya jimbo hilo na maafisa wa jimbo kukubali kushirikiana kwa kuwasalimisha wahamiaji waliokamatwa.
Marius Borg Hoiby, mwana wa Crown Princess wa Norway, ameiambia mahakama ya Oslo kuwa hakuwabaka wanawake wanne kama inavyodaiwa, akisisitiza kuwa mahusiano yote yalikuwa ya ridhaa licha ya mashtaka mazito…
Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, wamesifu ushirikiano thabiti wa kiuchumi, kisiasa na kiusalama kati ya nchi hizo mbili wakisema unatuliza hali katika nyakati hizi…
Watu wasiopungua 21 wanaripotiwa kuuawa na zaidi ya wengine 30 kujeruhiwa kutokana na mashambulizi ya Israel huko Gaza siku ya Jumatano baada ya mapigano kuanza upya katika eneo hilo la…
Katika juhudi za kuleta utulivu wa kudumu nchini Kongo, Umoja wa Afrika umeanzisha jopo maalum la upatanishi linalolenga kuratibu mazungumzo na kuhimiza ushirikiano wa kikanda. Ushiriki wa Museveni, Kenyatta, Obasanjo…
Wajumbe kutoka Moscow na Kyiv wamekutana leo mjini Abu Dhabi kwa awamu nyingine ya mazungumzo yanayosimamiwa na Marekani kuhusu kumaliza vita vilivyodumu takribani miaka minne.
Shirika la Msalaba Mwekundu limesema watu wenye silaha wamewauwa zaidi ya watu 168 katika jimbo la Kwara nchini Nigeria. Hayo ni ni miongoni mwa mashambulizi mabaya kutokea hivi karibuni.
Kansela wa Ujerumani, Merz, anazuru nchi tatu za Ukanda wa Ghuba ndani ya saa 72 tu. Katika ziara hiyo, kama alivyofanya awali nchini India, anatafuta ushirikiano mpya wa kimkakati wakati…
Waasi wa M23 wamekiri kuhusika na shambulizi la droni liliulolenga uwanja wa kimkakati wa ndege unaotumiwa na jeshi katika eneo la kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limesitisha shughuli zake katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Sudan Kusini baada ya msafara wake wa misaada kushambuliwa.
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz Jumatano anaanza ziara yake ya siku tatu ambayo ni ya kwanza katika eneo tajiri na lenye umuhimu wa kimkakati la Ghuba.
Shirika la Afya Duniani, WHO, limeomba dola bilioni moja za Marekani ili kukabiliana na majanga ya kiafya mwaka huu kwa ajili ya maeneo 36 yenye dharura zaidi duniani, huku watu…
Ripoti ya mwaka ya Human Rights Watch yafichua taswira ya kutisha ya ukiukaji wa haki za binadamu duniani, ikionyesha raia kama walengwa wakuu wa vita, siasa kandamizi na mifumo dhaifu…
Jeshi la Sudan limesema limeuvunja mzingiro wa miaka mingi katika mji wa Kadugli. Hatua hii ya sasa nchini Sudan inaashiria mabadiliko katika muelekeo wa vita vinavyoikumba nchi hiyo.
Ripoti ya kila mwaka iliyotolewa leo na Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW), inaonyesha kuwa mfumo wa kimataifa wa haki za binadamu uko hatarini.
Shirika la ulinzi wa raia la Gaza limesema mashambulizi ya anga ya Israel yamewaua watu tisa katika eneo la Wapalestina, ikiwemo watoto watatu.
Jeshi la Sudan limesema limeuvunja mzingiro wa miaka mingi katika mji wa Kadugli na kutoa matumaini kwa maelfu ya watu wanaokabaliwa na kitisho cha baa la njaa.
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, leo anaanza ziara yake ya kwanza katika eneo muhimu lenye utajiri na la kimkakati la Ghuba.
Wasuluhishi kutoka Ukraine, Urusi na Marekani wanatarajiwa kukutana leo mjini Abu Dhabi, wakitafuta kuendeleza mazungumzo tete ya namna ya kumaliza vita vya karibu miaka minne.
Watu wasiopungua 15 wamefariki baada ya boti ya doria ya walinzi wa pwani ya Ugiriki kugongana na boti iliyowabeba wahamiaji nje ya pwani ya kisiwa cha Chios Jumanne usiku.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema haki za binadamu zadorora. Marekani, Urusi, Iran na Afghanistan zatuhumihiwa, huku dhidi ya mashoga ikiongezeka.
Jopo maalumu la upatinishi la Umoja wa Afrika limesisitiza kuwa bara hilo linatakiwa kuhusika moja kwa moja katika kuutatua mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini sheria inayorefusha mkataba wa biashara kati ya Marekani na Afrika, AGOA, hadi Desemba 31 mwaka huu wa 2026.
Iran na Marekani zimethibitisha rasmi kwenda kwenye mazungumzo yanayolenga kuepusha makabiliano ya moja kwa moja kati yao, lakini bado Rais Donald Trump hajaondosha uwezekano wa hatua za kijeshi dhidi ya…
Marekani imerejesha fedha za mauzo ya mwanzo ya mafuta ya Venezuela, ikiwa ni sehemu ya makubaliano baina ya Caracas na Washington yaliyofikiwa mwezi uliopita, baada ya kupinduliwa na kutekwa Rais…
Mamlaka nchini Ugiriki zinasema watu 15 wamekufa kufuatia ajali ya kugongana kwa mashua ya walinzi wa pwani ya Ugiriki na ile ya wahamiaji kando ya ufukwe wa Kisiwa cha Chios…
Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa kiume wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, ameuawa kupitia kile ofisi yake ilichosema ni "tendo la kihalifu na la woga" katika mji wa magharibi…
Rais Donald Trump wa Marekani amesaini sheria ya kuongeza muda wa programu ya biashara yenye masharti nafuu kati ya nchi yake na Afrika hadi tarehe 31 Disemba mwaka huu.
Katika hatua isiyo ya kawaida, mahakama ya kijeshi nchini Brazil imetangaza azma ya kuanzisha uchunguzi utakaomua endapo itapaswa kumvua hadhi ya kijeshi rais wa zamani wa nchi hiyo, Jair Bolsonaro.
Wizara ya mambo ya nje ya Qatar imesema juhudi kubwa za kidiplomasia zinaendelea kati ya Iran, Qatar na mataifa mengine ya kikanda baada ya Tehran kuthibitisha mazungumzo na Marekani.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemteua bila kukusudia mtu aliyekufa kuwa mjumbe wa kamati itakayoandaa uchaguzi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Urusi imerejelea pendekezo lake kwa Marekani kuhusu kuendelea kutekeleza kwa mwaka mmoja zaidi, vipengele vya mkataba wa kupunguza silaha za nyuklia wa New START, unaomalizika Alhamisi.
Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema linahitaji kiasi cha dola bilioni moja mwaka huu kugharimia dharura za kiafya, magonjwa ya mlipuko na matibabu ya utapiamlo ulimwenguni.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameishutumu Eritrea hii leo kwa kile ilichotaja 'mauaji ya kimbari' wakati wa vita vya Tigray kati ya mwaka 2020-2022, wakati huo mataifa hayo yakiwa…
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amemwagiza waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo kufanya mazungumzo ya "haki na yenye usawa" na Marekani, ikiwa ni ishara ya kwanza ya wazi…
Huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea kuzuia mzozo mpana Mashariki ya Kati, Saudi Arabia, mataifa ya Ghuba na Israel zinaweka mbele maslahi yao wakati mvutano kati ya Marekani na Iran ukiendelea…
Wadau wengi wa soka waliofuatilia maandalizi na mafanikio ya AFCON 2025 nchini Morocco wametahadharisha kuwa Afrika Mashariki ina kazi kubwa ili kukidhi viwango vya juu vilivyoainishwa na wenyeji wa mashindano…
Kumeibuka mjadala kuhusu nia ya Rais Donald Trump kuanzisha vituo vya kijeshi vya Marekani katika kisiwa cha Greenland - hatua inayofanana na muundo wa vituo vya kijeshi vya Uingereza katika…
Umoja wa Mataifa utapeleka ujumbe wake wa kulinda amani nchini Kongo katika siku za hivi karibuni, kwa uangalizi wa juhudi za usitishaji vita kati ya serikali ya DRC na waasi…