Trump: Ukraine na Urusi zinakaribia makubaliano ya amani
Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kwamba Ukraine na Urusi ziko karibu kufikia makubaliano ya amani. Aliyasema hayo alipomkaribisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kwenye makazi yake ya Florida.