María Corina Machado ashinda Tuzo ya Amani ya Nobel
Kamati ya Nobel ya Norway, imemtangaza kiongozi wa upinzani Venezuela na mwanaharakati wa kutetea demokrasia Maria Corina Machado kuwa mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2025.
Kamati ya Nobel ya Norway, imemtangaza kiongozi wa upinzani Venezuela na mwanaharakati wa kutetea demokrasia Maria Corina Machado kuwa mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2025.
Chama tawala nchini Korea Kaskazini, Chama cha Wafanyakazi, kinaadhimisha miaka 80 tangu kuasisiwa kwake.
magenge ya wahalifu wamepambana na polisi aktika mji mkuu wa Haiti, Port-au.Prince. Milio ya risasi imeripotiwa mjini humo.
Algeria imefuzu kwa Kombe la Dunia siku ya Alhamisi, ikiwa ni timu ya nne kutoka Afrika kupata nafasi hiyo kwa mashindano yatakayofanyika Marekani Kaskazini mwakani, baada ya kuwafunga Somalia 3-0.
Rais Felix Tshisekedi ametoa wito kwa mwenzake wa Rwanda Paul Kagame "kukumbatia amani" na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Rais Recep Tayyip Erdogan ametangaza kuwa Uturuki iko tayari kushiriki katika ujumbe wa mataifa mbalimbali kufuatilia kusitishwa kwa mapigano Gaza, akiahidi kuunga mkono juhudi za ujenzi upya.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kiutu, OCHA imesema takribani tani 170,000 za misaada zimeandaliwa na zinasubiri kupelekwa katika Ukanda wa Gaza.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi amemtaka Rais wa Rwanda, Paul Kagame kuacha kuwaunga mkono waasi wa M23 nchini Kongo.
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen amesalimika katika kura mbili za kutokuwa na imani naye katika Bunge la Ulaya.
Jumuiya ya Maendeleo ya Biashara ya Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika — COMESA — imetangaza kuanza mkakati mkubwa wa kidijitali unaolenga kuimarisha biashara.