Mwenyekiti wa kamati ya Nobel ya Norway Jørgen Watne Frydnes, amesema Machado aliyekuwa mgombea urais wa upinzani nchini Venezuela, alisifiwa kwa kuwa kiungo muhimu cha kuunganisha upinzani wa kisiasa nchini humo ambao wakati mmoja ulikuwa umegawanyika sana na kuibuka na wito wa pamoja wa uchaguzi huru na serikali ya uwakilishi.

Frydnes ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka uliopita, Machado amelazimika kuishi mafichoni, lakini licha ya vitisho vikali dhidi ya maisha yake, alibakia nchini humo, chaguo ambalo limewahamasisha mamilioni ya watu.

Kumekuwa na uvumi unaoendelea kabla ya tangazo hilo la mshindi kuhusu uwezekano wa tuzo hiyo kumuendea Rais wa Marekani Donald Trump, ukichochewa kwa sehemu na Trump mwenyewe, na zaidi kwa kuidhinishwa wiki hii kwa mpango wake wa kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *