Korea Kaskazini leo inasherehekea miaka 80 ya chama tawala cha Wafanyakazi.

Vigogo na viongozi mbalimbali wa kigeni wanatarajiwa kuwa sehemu ya maadhimisho hayo, huku Urusi ikiwakilishwa na rais wa zamani Dmitry Medvedev, ambaye anahudumu kama naibu mkuu wa Baraza la Usalama linaloongozwa na rais Vladimir Putin.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa China Li Qiang siku ya Alhamisi mjini Pyongyang na kusifu “uhusiano wa kirafiki na ushirikiano” wa nchi hizo mbili, wakati Kim akisimamia sherehe za Chama cha Wafanyakazi.

Ziara ya Li imekuja wakati majirani hao wakitaka kudumisha uhusiano wa karibu licha ya muda wa uhusiano mbaya kati ya China na Korea Kaskazini kuhusu mpango wa nyuklia wa Pyongyang.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *