Hali hiyo imetokea wakati baa la njaa lililoripotiwa huko, likizidi kutoa shinikizo kwa Israel kuachana na vita vyake, ikiwa ni miezi 22 tangu ilipoanza kulishambulia kundi la Hamas. 

Waziri wa Ulinzi wa taifa  hilo, Israel Katz ameonya kuwa Gaza itasambaratishwa  katika operesheni mpya ya kijeshi iliyoidhinishwa hivi karibuni inayonuia kulidhibiti kikamilifu eneo hilo. 

Waziri wa maendeleo wa Ujerumani asema msaada zaidi unahitajika Gaza

Onyo hili limetolewa licha ya Shirika la kutathmini Usalama wa upatikanaji wa Chakula duniani, IPC, kutoa ripoti inayosema mji huo unakabiliwa na baa kubwa la njaa huku likionya hali inaweza kuwa mbaya zaidi iwapo vita havitositishwa.

Tangazo la baa la njaa Gaza, limekuja baada ya miezi kadhaa ya onyo kutoka kwa makundi ya misaada  kwamba hatua ya Israel kuzuwia chakula kuingia pamoja na mashambulizi yake ya kijeshi zinasababisha njaa miongoni mwa wapalestina hasa watoto. 

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekanusha ripoti ya IPC akiita ya uwongo. 
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *