
Afrika Kusini inazidi kuimarisha jukumu lake kama mpatanishi katika suala la vita nchini Ukraine. Kama mwenyekiti wa G20 mwaka huu, nchi hii inatumia jukwaa hili ili sauti yake iweze kusikika. Cyril Ramaphosa alianzisha mchakato wa mazungumzo ya simu na wakuu wa nchi za Ulaya. Mnamo Agosti 23, kwa mfano, alizungumza na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anazidi kupaza sauti juu ya suala la Ukraine, kama inavyoonyeshwa na mfululizo huu wa mazungumzo ya simu. Rais Ramaphosa alizungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, Rais wa Finland Alexander Stubb na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Wote hawa alizungumza nao kwa siku moja, Agosti 23, aripoti mwandishi wetu nchini Afrika Kusini, Valentin Hugues.
Msururu huu wa mazungumzo ya simu, haswa kusisitiza udharura wa kuandaa mkutano wa pande tatu kati ya Ukraine, Urusi, na Marekani, kwa ajili ya dhamira thabiti ya kukomesha vita. Majadiliano na viongozi wengine wa Ulaya yamepangwa katika siku zijazo, imetangaza ofisi ya rais wa Afrika Kusini. Imeongeza kuwa “viongozi hawa wa Ulaya wanathamini jukumua la Afrika Kusini katika mazungumzo,” kwa Afrika Kusini ni nchi isiyofungamana na upande wowote na inafanya kazi kama mpatanishi.
Ziara rasmi ya kwanza ya Zelensky katika nchi ya Kiafrika
Mwezi Aprili mwaka jana, Volodymyr Zelensky alifanya ziara rasmi mjini Pretoria, ziara yake ya kwanza rasmi katika bara la Afrika tangu kuanza kwa vita. Wakati wa mazungumzo yake ya simu na Cyril Ramaphosa mnamo Agosti 23, rais wa Ukraine alibainisha tena, kulingana na ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, “kuwa tayari kwa aina yoyote ya mkutano na mkuu wa nchi wa Urusi.” Pia aliishutumu Moscow kwa “kuchelewesha mambo” na kutoa wito kwa juluiya ya kimataifa “kutuma ishara zinazofaa na kuishinikiza Urusi kuelekea amani.”
Kama mwanachama wa BRICS, pamoja na Urusi, Afrika Kusini pia ni moja ya nchi adimu ambazo zinaweza kuzungumza na Kyiv na Moscow. Wiki iliyopita, kwa mfano, Cyril Ramaphosa alikutana na Vladimir Putin kutathmini mazungumzo ya amani. Alimwita rais wa Urusi “mshirika mpendwa” na “rafiki wa thamani” mnamo mwezi Oktoba katika mkutano wa kilele wa BRICS. Lakini, kwa mara ya kwanza tangu shambulizi la Urusi dhidi ya Ukraine, Afrika Kusini ilipiga kura mapema mwaka huu kwa azimio la Umoja wa Mataifa linaloelezea vita kama “uvamizi kamili wa Ukraine” na Urusi na “kuthibitisha tena kujitolea kwake” kwa “uadilifu wa eneo la nchi.”
Jukumu la upatanishi ambalo ni muhimu zaidi wakati sauti ya Afrika Kusini inapopazwa katika anga ya kimataifa mwaka huu, kama nchi mwenyeji wa mkutano ujao wa G20.