#HABARI: Mfanyabiashara maarufu Mjini Moshi, Bw#HABARI: Mfanyabiashara maarufu Mjini Moshi, Bw

#HABARI: Mfanyabiashara maarufu Mjini Moshi, Bw. Ibrahimu Shao, amechukua fomu ya kuwania Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Jimbo la Moshi Mjini.

Mgombea Ubunge huyo amekabidhiwa fomu na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Moshi Mjini, Ndugu Sifael Kulanga.

Baada ya kukabidhiwa fomu hiyo Bw.ibrahimu Shao, ameahidi kushirikiana na Wanacccm Moshi, katika kuhakikisha Chama hicho kinapata ushindi wa kishindo .

Akizungumza mara baada ya kukabidhi fomu hiyo ya Uchaguzi Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Moshi, Bw. Sifael Kulanga, amesema jumla ya wagombea tisa wa vyama mbalimbali tayari wameshachukua fomu .

#follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *