#HABARI: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Mhe#HABARI: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Mhe

#HABARI: Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Mhe. Waziri Kombo amepongeza ushirikiano wa Tanzania na Japan kupitia JICA katika ufadhili wa uendelezaji wa sekta za kilimo, nishati, usafirishaji, afya, maji na uendelezaji wa rasilimali watu.

Waziri Kombo amebainisha haya alipofanya mazungumzo na Bw. Ando Naoki, Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) pembezoni mwa Mkutano wa Tisa wa TICAD uliofanyika jijini Yokohama.

Katika kikao hicho walikubaliana kuendeleza ushirikiano huo hususani katika sekta za miundombinu bora, uendelezaji wa rasilimali watu, Uchumi wa Buluu na Kilimo, hususani teknolojia ya kuongeza thamani malighafi za mazao.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *