
Kiongozi Muadhamu wa Iran anaishutumu Marekani—mshirika wa Israel—kwa kutaka “kuitiisha” nchi yake na kuupindua utawala wake.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mvutano bado uko juu sana kati ya Washington na Tehran. Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ametoa wito jana Jumapili kuwepo kwa umoja katika kukabiliana na kile alichokitaja kuwa ni juhudi za Marekani za “kuitiisha” nchi yake.
Matamshi yake, yaliyochapishwa kwenye tovuti yake rasmi, ni miongoni mwa kauli zake adimu tangu usitishaji vita uliotangazwa na Washington Juni 24, ambao ulihitimisha vita vya siku kumi na mbili kati ya Israel na Iran.
Vituo vikuu vya nyuklia vilishambuliwa
Mnamo Juni 13, Israel ilianzisha mashambulizi dhidi ya Iran, kwa kushambulia kwa mabomu maeneo ya kijeshi na nyuklia na maeneo yenye watu wengi kwa siku kadhaa, na kuua zaidi ya watu 1,000. Kisasi cha Iran kilisababisha vifo vya Waisrael 29. Katikati ya mashambulizi ya Israel, Marekani ilishambulia maeneo muhimu ya nyuklia nchini Iran tarehe 22 Juni.
Kwa mujibu wa Ali Khamenei, mashambulizi haya yalilenga kuyumbisha Jamhuri ya Kiislamu. Mnamo Juni 13, “Iran ilishambuliwa. Siku iliyofuata, katika mji mkuu wa Ulaya, maafisa wa Marekani walikutana kujadili serikali ambayo inapaswa kuongoza Iran baada ya Jamhuri ya Kiislamu,” alitangaza, akisisitiza kwamba lengo la Washingtoni “ni Iran kuitii Marekani.”
Kabla ya mashambulizi ya Israel, Tehran na Washington walikuwa katika mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Iran. Mataifa ya Magharibi na Israel yanaishutumu Iran kwa kutaka kupata silaha za nyuklia, madai ambayo Tehran inakanusha, ikitetea haki yake ya kuwa nyukliahiyo ni kwa mpango wa kiraia.
Kukataa mazungumzo ya moja kwa moja
Ali Khamenei pia ameelezea mapendekezo ya mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani yaliyotolewa na sehemu ya kambi ya wanamageuzi yako “juu sana”. Kulingana na yeye, “mazungumzo hayatatatua matatizo yetu ikiwa mahitaji yatawasilishwa kwa Marekani.” Ali Khamenei, ambaye ndiye mwenye usemi wa mwisho kuhusu maamuzi yote ya kimkakati, pia ameonya dhidi ya “mkakati wa adui,” ambao alisema unalenga “kuchochea mifarakano” nchini Iran. “Kuna tofauti za kimtazamo, lakini linapokuja suala la kutetea mfumo na kumpinga adui, wananchi wanaungana,” amebainisha.
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tehran na Washington umevunjika kwa zaidi ya miaka arobaini.