Charles Kushner ameitakiwa kufika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa leo Jumatatu, Agosti 25, baada ya kueleza “wasiwasi wake mkubwa kuhusu kuongezeka kwa chuki dhidi ya Wayahudi nchini Ufaransa na ukosefu wa hatua za kutosha za serikali [yake] kukabiliana na tabia hiyo” katika barua kwa Emmanuel Macron.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Charles Kushner, balozi wa Marekani nchini Ufaransa, ameitwa kuripoti katika Wizara ya Mambo ya Nje siku ya Jumatatu, Agosti 25, baada ya kukosoa Rais Emmanuel Macron kwa “kutochukua hatua za kutosha” dhidi ya chuki kwa Wayahudi, jambo ambalo limeikasirisha Paris. Katika barua iliyotumwa kwa mkuu wa nchi ambayo shirika la habari la AFP limeoata kopi siku ya Jumapili, balozi huyo anaonyesha “wasiwasi wake mkubwa juu ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya Wayahudi nchini Ufaransa na ukosefu wa hatua za kutosha za serikali [ya Ufaransa] kukabiliana na taia hiyo,” akirejelea ukosoaji ambao tayari umetolewa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Yakichukuliwa kama shutuma “zisizokubalika”, matamshi haya “yalikanushwa vikali” na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa: “yanakinzana na sheria za kimataifa, haswa jukumu la kutoingilia masuala ya ndani ya nchi […]. [Haya] pia hayaakisi ubora wa uhusiano wa Atlantiki kati ya Ufaransa na Marekani na uaminifu ambao lazima utokee kati ya Washiriki wote,” “Balozi Kushner ataitwa […] siku ya Jumatatu, Agosti 25” – hatua ambayo ni nadra sana kati ya nchi hizi mbili washirika.

Ukosoaji huo kutoka kwa mwanadiplomasia huyo wa Marekani, ambaye hivi karibuni alianza kazi yake mjini Paris, unakuja siku chache baada ya Benjamin Netanyahu kumshambulia kwa nguvu rais wa Ufaransa, akimtuhumu “kuchochea moto dhidi ya Wayahudi kwa kutoa wito wa kutambuliwa kimataifa kwa taifa la Palestina.” Ofisi ya rais wa Ufaransa ilikuwa tayari imejibu uchanganuzi huu kwa kuuelezea kama “upotovu, mbaya, na [ambao] hautapita bila kujibiwa.”

“Hakuna nafasi tena ya usawa”

Katika barua yake ya Jumatatu, Agosti 25, balozi wa Marekani aliunga mkono hoja ya Benjamin Netanyahu. “Kauli zinazoidhalilisha Israel na ishara za kutambua taifa la Palestina zinahimiza watu wenye msimamo mkali, kuchochea ghasia, na kuhatarisha Uyahudi nchini Ufaransa,” alisema Charles Kushner, baba wa mkwe wa Donald Trump, Jared Kushner, na kuongeza: “Leo, hakuna nafasi tena ya usawa: chuki dhidi ya Uzayuni, ni kupinga Uyahudi.” “Hakuna siku inapita nchini Ufaransa bila Wayahudi kushambuliwa mitaani, masinagogi na shule kuharibiwa, na biashara zinazomilikiwa na Wayahudi kuharibiwa. Wizara ya Mambo ya Ndani ya serikali yako inabainisha kuwa shule za chekechea zimekuwa zikilengwa kwa uharibifu dhidi ya Wayahudi,” aliongeza, wakati vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi vimekuwa vikiongezeka nchini Ufaransa tangu Oktoba 7, 2023 tarehe ya mashambulizi ya awali ya Hamas dhidi ya Israel, na kuzuka kwa vita huko Gaza.

Mwakilishi wa Marekani nchini Ufaransa pia amekasirishwa kuwa “karibu nusu ya vijana wa Ufaransa wanasema hawajawahi kusikia kuhusu mauaji ya Holocaust.” Akisifu hatua za Rais Trump katika suala hili na uwezo wake wa “kupambana na chuki dhidi ya Wayahudi, mradi tu viongozi wetu wana nia ya kuchukua hatua,” Charles Kushner anamtaka rais wa Ufaransa “kuchukua hatua kwa uthabiti.” “Kuongezeka kwa vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi nchini Ufaransa tangu Oktoba 7, 2023, ni tabia ambayo inatuumiza na ambayo mamlaka ya Ufaransa inaonyesha uhamasishaji kamili, kwani vitendo hivi havivumiliki,” imejibu Wizara ya mambo ya Nje ya Ufaransa.

Barua hii kutoka kwa balozi wa Marekani mjini Paris imetumwa kwa Rais Emmanuel Macron, ambaye alitangaza mwishoni mwa mwezi Julai kwamba Ufaransa italitambua taifa la Palestina katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba. Kufuatia hali hiyo, zaidi ya nchi kumi za Magharibi, zikiwemo Canada na Australia, zilitoa wito kwa nchi nyingine duniani kufanya hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *