Wadephul amesema hayo alipokutana na mwenzake wa Croatia Gordan Grlić Radman katika mji mkuu Zagreb, akisema Putin atakuwa anajidanganya, ikiwa anadhani atacheza na muda.

“Lazima tuendelee kuishinikiza Urusi. Ndiyo maana, ndani ya Umoja wa Ulaya, tunatayarisha awamu ya 19 ya vikwazo dhidi ya Urusi. Kwa hili sisi sote tunakubaliana kabisa. Ni umoja huu na uwazi ndio unaamua kuhusu bara letu. Kwa maana nguvu zetu zimo ndani yetu. Ulaya sio tu soko kubwa zaidi ulimwenguni; Ulaya pia ni ahadi ya usalama, ustawi na uhuru.”

Wakati huo huo, Wadephul amesisitiza msimamo wa Ulaya kwamba hakutafanyika makubaliano bila ya Ukraine, huku akiahidi kuendelea kuisaidia Ukraine kiuchumi, kijamii na kijeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *