Jeshi la DRC, FARC linaendelea kusakamwa na wasaizi wake kutoka kutoka makundi ya Wazalendo. Makabiliano yametokea tena siku ya Jumanne, Agosti 26, huko Uvira, Kivu Kusini. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa siku ya pili mfululizo, jeshi la Kongo, FARDC, wameendelea kukabiliana na wasaidizi wake Wazalendo, washirika wao katika vita vinavyoendelea. Idadi ya waliouawa, kwa mujibu wa jeshi hilo, ni mmoja aliyefariki upande wa FARDC, na watano waliouawa upande wa Wazalendo, pamoja na wengi wengi waliojeruhiwa. Hayo yote yalianza asubuhi ya Agosti 25, wakati Wazalendo walipozuia msafara wa abiria kutoka nchi jirani ya Burundi, wakati tayari mwishoni mwa wiki iliyopita, mapigano makali yamekuwa yakiendelea katika nyanda za juu zinazozunguka Uvira.

Mapigano kati ya FARDC na Wazalendo yalitokea katika eneo la Kivimvira, karibu kabisa na mpaka kati ya DRC na Burundi Agosti 26. Kwa mujibu wa jeshi la Kongo, wale wanaoitwa “wazalendo wasiotaka kuwa chini ya amri ya jeshi” walishambulia kikosi cha FARDC, brigedi ya “Panther” iliyopewa jukumu la kulinda mpaka huu.

FARDC yajibu kufuatia mashambulizi ya Wazalendo

Hili lilikuwa jibu la mapigano ya siku iliyotangulia, kwani mnamo Agosti 25, kitengo hiki cha jeshi kiliingilia kati huku hali ikizidi kuwa mbaya. Wapiganaji wa kundi moja la Wazalendo walizuia msafara wa mabasi kutoka Bujumbura yaliyokuwa yamewabeba Banyamulenge, jamii ya Wakongo waozungumza Kinyarwanda, kutoka mashariki mwa Kongo, waliokuja kumzika mmoja wao, afisa wa Kongo aliyefariki katika ajali ya ndege karibu na Kisangani.

Kwa hiyo jeshi la Kongo liliingilia kati. Lakini FARDC na Wazalendo walirushiana risase za moto. Hatimaye, mvutano ulikuwa mkubwa na mabasi yalirudishwa nyuma na mazishi ya afisa huyo wa jeshi mwenye cheo cha kanali yaliahirishwa kwa muda usiojulikana.

Hofu yatanda

Wazalendo wanasema wanahofia kupenya kwa Banyamulenge kupitia mpaka huu, huku wikendi nzima AFC/M23 wakionekana kujaribu kuuzunguka mji wa Uvira kwa kupitia maeneo jirani ili kuungana na Twirwaneho, kundi la kujilinda la Banyamulenge lenye mfungamano rasmi na AFC-M23. Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi hilo Reagan Mbuyi, Wazalendo kumi na wanne pia walikamatwa na kisha kukabidhiwa kwa kamanda wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *