Chanzo cha picha, SAFE
Mabilionea ulimwenguni wanakumbatia dhana mpya katika ujenzi wa makazi yaliyoundwa mahususi ili kuwalinda mabilionea hawa dhidi ya hatari inayowezekana inayosababishwa na vita, athari za mabadiliko ya tabianchi na vitisho vingine vya ulimwengu. Naam, tunazungumza kuhusu ‘makazi ya kifahari’ hapa.
Tofauti na makazi ya kawaida ya chini ya ardhi ambapo jambo muhimu zaidi ni kuhakikisha usalama na maisha ya watu, sekta hii inawekeza katika vituo vilivyoimarishwa ambavyo vitakuwa na orodha ndefu ya starehe na huduma.
Katika vyumba hivi vya kifahari, mabilionea hupata vitu kama huduma za urembo kama vile spars, vyakula vya asili na mandhari ambayo yanaonekana kama halisi ya ulimwengu wa nje. Haya yote ni mambo ambayo hufanya makazi haya kuwa mahali pa kuvutia.
Makazi haya yamebadilisha hali ya ‘maisha katika nyakati za mwisho’ kuwa hisia kama likizo ya kifahari katika hoteli ya kifahari ya chini ya ardhi .
Miaka michache iliyopita, mmiliki wa Meta Mark Zuckerberg alivuta hisia za ulimwengu kwa kutangaza mpango wake wa kujenga jengo kubwa huko Hawaii na miundombinu ya kukabiliana na majanga ya asili.
Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos pia amewekeza katika tahadhari sawa na hii.
Chanzo cha picha, SAFE
Soko la anasa la makazi ya kifahari linaonekana kushamiri kwao.
Hivi majuzi, kampuni ya Kimarekani ya Safe ilitangaza mipango ya kujenga ‘makao ya kimataifa’ zaidi ya 1,000, au vyumba vya chini ya ardhi, vilivyoko katika miji mbalimbali duniani.
Katika mahojiano na BBC News Brazil, mkurugenzi wa operesheni na udhibiti wa matibabu wa kampuni hiyo, Naomi Corby, alisema mradi huo unaoitwa Aerie, ikimaanisha neno la Kiingereza linalomaanisha kiota cha tai. Unafanya kazi kama klabu kwa wanachama wa kipekee.
“Uanachama ni kwa mwaliko tu na kwa wachache waliochaguliwa. Siwezi kushiriki maelezo mengi, lakini sio kwa kila mtu,” alielezea.
Gharama za kutumia makazi haya , hasa yaliyoundwa kwa ajili ya kuishi katika maafa makubwa, hutegemea ukubwa wa eneo lililochaguliwa.
Ikiwa ni makazi ya mita za mraba 185, yatagharimu takriban dola milioni 2, lakini kwa malazi makubwa zaidi bei inaweza kufikia dola milioni 20.
Kulingana na Corby, vituo vyote vina huduma za maji, chakula, malazi na matibabu bila kikomo.
“Sio lazima kutegemea mifumo ya taifa kwa ajili ya umeme.”
Hatua za usalama na ‘magereza ya ndani’
Mkurugenzi wa Safe anasema makazi haya yaliundwa kutengwa chini ya ardhi kwa muda mrefu na walikuwa na mikakati iliyojengwa ndani yakekwa hali ya migogoro kati ya timu za huduma, ikiwa ni pamoja na ‘gereza la ndani’.
“Siku zote kuna uwezekano wa tabia isiyotarajiwa au isiyokubalika. Hatua kadhaa za dharura zimewekwa katika makao hayo. Miongoni mwake ni gereza ambalo liko katika kila makazi.”
Kulingana na Corby, gereza hilo ‘litafanya kazi kama kituo chochote cha hali ya juu.’
‘Ni chumba kilichoundwa kuwaweka watu pekee, lakini ambapo mawasiliano na mwingiliano vinawezekana.’
Uamuzi wa nani atazuiliwa utakuwa ni kwa hiari ya mtumiaji.
Chanzo cha picha, SAFE
Kulingana na saizi, bei za makazi zinaweza kufikia hadi $20 milioni.
Makazi ya Erie yameanzishwa kama SCIFS (Kifaa Nyeti cha Taarifa za Sehemu), kumaanisha kwamba yana ulinzi mkali sana, na miundo inalindwa na ufuatiliaji wa kielektroniki, sawa na chumba cha migogoro cha White House.
Corby anakadiria kuwa mahitaji ya maeneo haya ya kifahari yanaongezeka kutokana na changamoto za sasa za kijiografia.
“Ubinadamu uko kwenye njia hatari, umefungwa kwa njia ya kidijitali na kudhibitiwa kabisa, bila suluhu inayoonekana,” anasema.
‘Makazi yaErie yanajitawala, ambapo usiri unatawala, ufikiaji hauna kikomo na wenye mamlaka wanayafurahia.’
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi