Vyama 17 kati ya 18 vimetimiza masharti ya kuanza kampeni za urais kabla ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 nchini Tanzania. Wagombea walioteuliwa na tume huru ya uchaguzi INEC wamepewa magari, madereva na ulinzi wa kutosha ili kutimiza azma yao.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tume huru ya taifa ya uchaguzi INEC imewateuwa wagombea 17 wa urais ambao kuanzia leo Alhamisi mwaka 2025, wataanza harakati za kampeni kwa siku 61 kuisaka Ikulu.

Uchaguzi wa mwaka huu unafanyika wakati chama kikuu cha upinzani Chadema kikiwa nje, kutokana na madai ya kusisitiza sharti la kufanyika marekebisho kwenye mfumo wa uchaguzi ili kuwapa na uchaguzi huru haki na unaoaminika.

Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, wakati akiwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Tanzania, Tarehe 2 Juni 2025.
Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, wakati akiwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Tanzania, Tarehe 2 Juni 2025. REUTERS – Emmanuel Herman

Mgombea wa chama cha Alliance democratics Change ADC Wilson Elias, ameenguliwa  katika mbio za urais kwa maelezo kuwa amekiuka taratibu za za kisheria katika mchakato wa uteuzi wa ndani wa chama.

Upande wake mgombea wa chama cha ACT Wazalendo amekutana na kizaa zaa baada ya kuondolewa kwenye kiny’anganyiro hicho kwa sababu za kutotimiza masharti ya chama ambapo kanuni ya chama hicho inadai mgombea mwanachama anayetaka kugombea nafasi ndani ya chama hicho kuwa amejiunga angalau siku saba kabla ya muda wa kutangazwa kwa mchakato wa uchaguzi, ambapo mmoja wa wafausi wa chama hicho aliwasilisha pengamizi la uteuzi wa mpina kuwa mgombea siku chache baada ya kukihama chama tawala CCM.

Aliyekuwa mgombea wa urais Luhaga Joelson Mpina kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo
Aliyekuwa mgombea wa urais Luhaga Joelson Mpina kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo © ACT Wazalendo

Kwa mantiki hiyo tunatarajia kuona Chama cha CCM ambacho kimemsimamisha rais Samia Suluhu Hassan akichuana na Gombo Samandito Gombo wa chama cha CUF, Haji Ambarty wa chama cha NCCR Mageuzi, Salum Mwalimu wa chama cha ukombozi wa umma Chauma, Saum Hussein Rashida wa chama cha UDP , Yustas Mbatina Rwamugira wa chama cha TLP, Abdul Juma Mluya wa chama cha Democrafic Party DP  na Coaster Jimmy Kibonde wa chama cha Makini, Geroge Gabriel Busungu wa chama cha TADEA, Mwajuma Noty Mirambo wa chama UMD, Twalib Ibrahim Kadege wa chama UPDP pamoja na Hassan Kisabya Almas wa chama cha NRA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *