Nchini Kenya, miili mitano mipya ilifukiliwa jana, Jumatano, Agosti 27, huko Kwa Binzaro, kijiji kidogo kwenye pwani ya Kenya, kulingana na shirika la kutetea haki za binadamu la Vocal Africa. Hii inafikisha 24 idadi ya miili iliyopatikana katika siku tano za utafutaji. Makaburi ya watu wengi yaligunduliwa siku kumi zilizopita na polisi, ambao wanashuku dhehebu jipya. Kulingana na hati za kipekee zilizopatikana na RFI, kuna uhusiano na dhehebu la Paul Mackenzie.
