#HABARI: Chama cha ACT Wazalendo Jimbo la Mbulu Vijijini, Mkoani Manyara, kimelaani kikundi cha vijana kinachotumika vibaya kis…#HABARI: Chama cha ACT Wazalendo Jimbo la Mbulu Vijijini, Mkoani Manyara, kimelaani kikundi cha vijana kinachotumika vibaya kis…

#HABARI: Chama cha ACT Wazalendo Jimbo la Mbulu Vijijini, Mkoani Manyara, kimelaani kikundi cha vijana kinachotumika vibaya kisiasa kupinga uteuzi wa Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbulu Vijijini, kwa tiketi ya chama hicho Bw. Flatei Gregory, na kudai kuwa taratibu zote za uteuzi ndani ya chama zilifuatwa ili kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 31 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Jimbo la Mbulu Vijijini, Bw. Thomas Moses, amesema kuwa vijana hao sio wanachama bali wanatumika vibaya kumchafua mgombea pamoja na chama hicho hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Katibu wa chama hicho Bw. Emanuel Lenga, amesema mgombea wa chama hicho ana sifa za kuwa kiongozi bora na kuwatumikia wananchi wa mbulu iwapo atapata ridhaa.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *