
Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), inayojumuisha mataifa 10 yakiwemo China, India, Urusi na Iran, imesema leo Jumatatu, Septemba 1, kwamba “inalaani vikali vitendo vinavyosababisha vifo vya raia” katika Ukanda wa Gaza na kutaka kusitishwa kabisa kwa mapigano, katika taarifa iliyochapishwa na shirika la habari la Xinhua.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
SCO pia “inalaani vikali” mashambulizi yaliyofanywa na Israel nchini Iran mnamo mwezi Juni, katika taarifa hii iliyotolewa mwishoni mwa mkutano wa kilele wa shirika hilo huko Tianjin (kaskazini).
Kwa hivyo, nchi wanachama “zinalaani vikali vitendo vinavyosababisha vifo vya raia na maafa ya kibinadamu huko Gaza” na “kutoa wito wa usitishaji vita kamili na wa kudumu na ufikiaji usiozuiliwa wa misaada ya kibinadamu,” inasema SCO.
Kwa kuongeza, “wanalaani vikali mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa mwezi Juni 2025 na Israel na Marekani kulenga miundombinu ya nyuklia ya kiraia kwa gharama ya majeruhi, (na) ukiukaji wa sheria za kimataifa na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa,” inaongeza.