
Zaidi ya miezi sita kabla ya uchaguzi wa rais nchini Congo-Brazzaville, mchakato wa mapitio ya orodha ya wapiga kura umeanza siku ya Jumatatu, Septemba 1. Utaendelea kwa miezi miwili.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu huko Brazzaville, Loïcia Martial
Kwa kutazamia uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Machi 2026, Congo-Brazzaville imezindua mapitio ya orodha yake ya wapiga kura siku ya Jumatatu, Septemba 1, kama inavyothibitishwa na mabango yanayotangaza mchakato huo yaliyobandikwa katika mji mkuu mzima.
Kama, katika manispaa ya mji wa Bacongo, eneo la pili kwa ukubwa la Brazzaville, vibao ambavo orodha hizo huwekwa kwa kawaida vilikuwa bado havijajazwa jana adhuhuri, wakati tume inaundwa, maofisa wawili waliokuwepo hapo hata hivyo wamesisitiza juu ya umuhimu wa marekebisho kama haya: “Lazima tufanye hivi ili kuwafahamisha watu, ili kila mtu ajue kuwa kutakuwa na uchaguzi wa urais mnamo mwaka 2026,” anasema. “Jina [la kila raia] lazima lionekane kwenye orodha ili kila mtu aweze kupiga kura. Ikiwa halipo, haiwezekani,” anaongeza mwenzake.
Marekebisho mazuri kwa uwazi wa kura
Katika eneo la kwanza, huko Makélékélé, orodha tayari zimewekwa kwenye vibao. Laurent Edgard Bassoukissa, meya ambaye ni mwenyekiti wa tume ya kurekebisha orodha, ameweka kila kitu mahali pake. “Tulichukua hatua zinazohitajika ili kuwafahamisha wakazi kuwa operesheni hiyo inaanza leo. Viongozi wa vitongoji walieneza habari hiyo kupitia wapiga kelele wa mijini,” anasema.
Akiwa mpiga kura, Dieu-Merci anasifu uhalali wa marekebisho haya: “Hii ni taarifa inayokaribishwa ili kujua wapiga kura waliofariki, ili uchaguzi ujao ufanyike kwa uwazi kabisa,” anasema.
Wakati wa uchaguzi uliopita wa urais uliofanyika nchini Jamhuri ya Kongo, mwaka 2021, nchi hiyo ilikuwa na wapiga kura zaidi ya milioni 2.645. Wananchi wa Kongo wana hadi Oktoba 30 kuhakikisha kuwa wamesajiliwa ipasavyo kwenye orodha ya wapiga kura.