Maporomoko makubwa ya udongo kwenye eneo la Darfur Magharibi nchini Sudan, yamesababisha maafa makubwa ikiwemo kufunika kabisa vijiji na kuua watu zaidi ya elfu 1, imesema taarifa ya kundi la Sudan Liberation Movement, linaloongoza eneo hilo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Maafa haya yameripotiwa baada ya siku kadhaa za mvua kubwa, ambapo kijiji cha Tarasin kilichoko katika milima ya Marra, kilifunikwa kabisa, waasi hao wamethibitisha.

Kundi hilo sasa linatoa wito kwa umoja wa Mataifa na mashirika mengine, kuwasaidia raia walioathiriwa ikiwemo operesheni za uokoaji na utafutaji wa miili ya watu waliofunikwa na vifusi vya udongo.

Sudan inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF, vita ambayo imeiingiza nchi hiyo katika moja ya majanga mabaya zaidi ya kibinadamu duniani.

Licha ya kundi la SLM kujitenga na mapigano yanayoendelea, lakini linadhibiti sehemu kubwa ya safu ya milima mirefu zaidi nchini Sudan.

Sehemu kubwa ya jimbo la Darfur, ikiwa ni pamoja na eneo ambako maporomoko ya ardhi yameripotiwa,  bado mashirika ya kibinadamu yanashindwa kufika kutokana na mapigano yanayoendelea, na hivyo kuzuia kwa kiasi kikubwa utoaji wa msaada wa dharura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *