.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Putin wa Urusi na mwenzake wa Ukraine Volodymir Zelensky

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, katika
mahojiano na ABC News, amekataa tena pendekezo la Rais wa Urusi Vladimir Putin
kwenda Moscow kwa mazungumzo ya amani.

“Anaweza kuja Kiev,” Zelensky alisema.
“Siwezi kwenda Moscow wakati nchi yangu inakabiliwa na mashambulizi ya
makombora kila siku. Siwezi kwenda kwenye mji mkuu wa gaidi huyu,” rais wa
Ukraine aliongeza.

Zelensky, akisisitiza juu ya mazungumzo katika
ngazi ya wakuu wa nchi, amerudia kusema kwamba Putin hataki kukutana naye,
kwani anaendelea kufanya vita nchini Ukraine.

Siku ya Jumatano, baada ya ziara nchini Uchina,
rais wa Urusi alisema kwamba “ikiwa Zelensky yuko tayari, aje
Moscow.” Zelensky alijibu Alhamisi huko Paris, ambapo alikuwa kwenye
mkutano wa kilele wa “muungano wa walio tayari.”

“Nadhani ikiwa unataka mkutano usifanyike,
unapaswa kunialika Moscow. Nadhani kwamba Urusi imeanza kuzungumza juu ya
mkutano – hiyo tayari si mbaya. Lakini hadi sasa hatuoni nia yao ya kumaliza
vita,” rais wa Ukraine alisema.

Putin aliendelea kusisitiza mjini Vladivostok siku
ya Ijumaa kwamba Moscow ndiyo chaguo pekee la mazungumzo.

“Sikiliza, upande wa Ukraine unataka mkutano huu na unapendekeza mkutano huu. Nilisema: Niko tayari, tafadhali njoo, kwa hakika tutatoa masharti ya kazi na usalama, dhamana ya 100%,” rais wa Urusi alisema. “Ninarudia tena: ikiwa mtu anataka kweli kukutana nasi, tuko tayari. Mahali pazuri zaidi kwa hili ni mji mkuu wa Shirikisho la Urusi, jiji la shujaa la Moscow.”



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *