Chanzo cha picha, Anadolu via Getty Images
Jeshi la
Israel limeharibu jengo la pili kwa urefu katika mji wa Gaza, kama lililokuwa
imelilenga.
Waziri wa
Ulinzi Israel Katz aliweka video ya jengo hilo likiporomoka kwenye mtandao wa X,
na nukuu: “Tunaendelea”.
Jeshi la
Ulinzi la Israeli (IDF), ambalo limekuwa likipanua operesheni zake huko Gaza,
lilisema jengo la Sussi lilikuwa linatumiwa na Hamas – madai ambayo
yamekanushwa na kundi hilo la wanamgambo.
Haikuweza kufahamika mara moja iwapo kulikuwa na
majeruhi. Kabla ya shambulizi la Jumamosi, Israel ilidondosha vipeperushi
vinavyorudia wito wa Wapalestina kuhama katika kile inachokiita eneo la
kibinadamu kusini.