[ad_1]

h

Chanzo cha picha, Reuters

Hamas imedai imesema kuwa viongozi wake waliolengwa na shambulizi la anga la Israel wamenusurika , lakini watu sita wameuawa
katika shambulio hilo.

Wakati huo huo Rais
wa Marekani Donald Trump amesema “hajafurahishwa” na mashambulizi ya
anga ya Israel huko Qatar, na kuongeza shinikizo la kimataifa baada ya
kuongezeka kwa vita vya Israel dhidi ya Hamas.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
alisema mashambulizi hayo yalikuwa “halali kabisa” kwa sababu uyaliwalenga
viongozi wakuu wa Hamas ambao walipanga
shambulio la tarehe 7 Oktoba 2023 dhidi ya Israeli, ambalo lilianzisha vita vya
Gaza.

Kundi la
wapiganaji wa Palestina limesema wanachama wake watano waliuawa katika
shambulio la anga la Israel katika mji mkuu wa Qatar, lakini lilidai kuwa
jaribio la kuua timu yake ya mazungumzo “lilifeli”.

Qatar ililaani
shambulizi hilo la Israel, na kuliita la “uoga” na “ukiukaji wa
wazi wa sheria za kimataifa”.

Qatar ni mshirika
mkuu wa Marekani katika eneo ambalo ni eneo la kituo kikuu cha anga cha
Marekani.

Alipoulizwa
kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya Qatar, Trump alisema: “Sawa,
sifurahishwi… sijafurahishwa na hali nzima. Sio hali nzuri.

“Lakini
nitasema hivi, tunataka mateka warejeshwe, lakini hatujafurahishwa na jinsi
ilivyoshuka leo,” aliambia vyombo vya habari.

Hamas ilisema
timu ya mazungumzo ilikuwa inakutana kujadili pendekezo la hivi punde la
Marekani la kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza katika makazi ya watu huko
Doha wakati liliharibiwa vibaya na mfululizo wa milipuko.

Wizara ya mambo
ya ndani ya nchi hiyo ya Ghuba imesema mwanajeshi mmoja wa kikosi chake cha
Usalama wa Ndani aliuawa na wengine kujeruhiwa, bila kutaja majeruhi wowote wa
Hamas.

Qatar imekuwa
mwenyeji wa ofisi ya kisiasa ya Hamas tangu 2012, na imehudumu pamoja na
Marekani na Misri kama mpatanishi katika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja
kati ya kundi hilo na Israel.

[ad_2]

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *