[ad_1]

Picha nyeusi na nyeupe ya Bob Marley akiwa kwenye kiti cha abiria cha gari na mwili wake ukiwa umegeuzwa sehemu ya nyuma ya gari.

Chanzo cha picha, Dennis Morris

Maelezo ya picha, Dennis Morris alichukua picha hii, inayoitwa Babylon by van, wakati wa ziara ya kwanza ya Bob Marley nchini Uingereza

    • Author, Tim Stokes
    • Nafasi, BBC News

Mapema alfajiri mwaka 1973, kijana mwenye umri wa miaka 14 aitwaye Dennis Morris alifanya uamuzi ambao ungebadili maisha yake milele.

“Bob Marley alikuwa anakuja kufanya ziara yake ya kwanza nchini Uingereza, nami nikaamua kwamba nataka kumpiga picha. Nikatoroka shule na kuelekea kwenye klabu aliyokuwa anatumbuiza kwa mara ya kwanza jijini London.”

“Alipokuwa akitembea kuelekea nilipokuwa, nikamwambia: ‘naweza kukupiga picha?’ Akanijibu: ‘Ndiyo ndugu, ingia ndani.'”

Wakati wa mapumziko ya ukaguzi wa sauti, Marley alianza kuzungumza na Dennis kuhusu maisha ya kukua Uingereza, huku kijana huyo naye akimhoji kuhusu maisha yake nchini Jamaica.

[ad_2]

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *