Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Manchester United inataka kumsajili kiungo wa kati wa Nottingham Forest na England mwezi Januari Elliot Anderson, 22. (Teamtalk)
Arsenal imepiga hatua katika mazungumzo ya kurefusha mikataba ya winga wa Uingereza Bukayo Saka,24, na beki wa Ufaransa William Saliba,24, mikataba hiyo itakapomalizika mwishoni mwa msimu wa 2026-27. (Teamtalk)
Kipa wa Cameroon Andre Onana, ambaye anakaribia kujiunga na Trabzonspor ya Uturuki kwa mkopo, alikataa ofa kutoka kwa vilabu kadhaa – ikiwa ni pamoja na Monaco – msimu wa kiangazi baada ya mchezaji huyo wa miaka 29 kuambiwa atakuwa chaguo la kwanza la kocha wa Manchester United Ruben Amorim msimu huu. (The i Paper – Usajili unahitajika)
Beki wa Manchester United na Uholanzi Tyrell Malacia, 26, anaweza kutolewa mkopo wa msimu mzima katika klabu ya Uturuki ya Super Lig Eyupspor. (Sun)
Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyomfuatilia beki wa Ajax Mholanzi Aaron Bouwman, 18. (Teamtalk)
Hamburg wana chaguo kubadilisha usajili wa mkopo wa kiungo wa kati wa Ureno Fabio Vieira, 25, kutoka Arsenal kuwa mkataba kudumu kwa €20m (£17.3m). (Bild, via Goal)
Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania na mlinzi wa zamani wa Manchester City Aymeric Laporte, 31, anasubiri uamuzi wa Fifa kuhusu uhamisho wake wa Athletic Bilbao kutoka Al-Nassr baada ya kushindwa katika usajili wa majira ya kiangazi. (AS – kwa Kihispania)
Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Uingereza Josh Brownhill, 29, amekamilisha uchunguzi wa afya katika Al-Shabab na anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo ya Saudia kwa uhamisho wa bure baada ya kuondoka Burnley mwishoni mwa msimu uliopita. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 33, alikuwa akihusishwa na uhamisho wa Saudi Arabia lakini Manchester United inaweza kusalia naye hadi kandarasi yake itakapokamilika msimu ujao kwa kuwa amekuwa sehemu muhimu ya timu ya meneja Ruben Amorim. (Caught Offside)
Inter Milan ilionyesha nia ya kumnunua mshambuliaji wa Canada Jonathan David kabla ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kujiunga na Juventus kwa uhamisho wa bila malipo baada ya kuondoka Lille msimu wa kiangazi. (Gazzetta dello Sport – kwa Kiitaliano)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi