William Saliba

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal imempa beki wa Ufaransa William Saliba nyongeza ya kandarasi ya miaka mitano huku ikiendelea kujadiliana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika 2027. Real Madrid wanafuatilia hali ya beki huyo wa kati. (FootMercato – kwa Kifaransa)

Liverpool ina imani kuwa inaongoza katika mbio za kumsajili beki wa Uingereza Marc Guehi, 25, msimu ujao wa kiangazi wakati mkataba wa beki huyo wa Crystal Palace utakapokamilika na wanaandaa dau la la pauni milioni 87 kumsaini winga wa Bayern Munich na Ufaransa Michael Olise, 23. (Caught Offside)

Mgombea urais wa Benfica Joao Noronha Lopes anataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Manchester City Bernardo Silva mwezi Januari endapo atachaguliwa na tayari amefanya mazungumzo na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 31, ambaye mkataba wake utamalizika msimu ujao. (Record – kwa Kireno)

Manchester United inawakagua mabeki wa Uingereza Harry Maguire, 32, na Luke Shaw, 30, wakati ikijiandaa kuimarisha safu yake ya ulinzi msimu ujao. (Teamtalk)



Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *