[ad_1]

Umati wa Wapalestina wamekusanyika katika kituo cha usambazaji wa misaada karibu na kivuko cha mpaka cha Zikim cha Gaza, kilichozungukwa na vifusi na majengo yaliyolipuliwa.

Chanzo cha picha, Khames Alrefi/Anadolu via Getty Images

Maelezo ya picha, Umati wa Wapalestina wamekusanyika katika kituo cha usambazaji wa misaada karibu na kivuko cha mpaka cha Zikim cha Gaza, kilichozungukwa na vifusi na majengo yaliyolipuliwa.

    • Author, Luis Barrucho
    • Nafasi, BBC World Service

Vita vya Gaza vimeibua mjadala wa kimataifa kuhusu iwapo Israel inafanya mauaji ya halaiki, ambayo inachukuliwa na wengi kuwa uhalifu mkubwa zaidi chini ya sheria za kimataifa.

Kufikia katikati ya mwezi Agosti, mashambulizi ya kijeshi ya Israel yameua zaidi ya watu 61,000 – wengi wao wakiwa raia huko Gaza, kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas.

Mashambulizi hayo yalizinduliwa kujibu mashambulizi ya Hamas tarehe 7 Oktoba 2023, ambapo wengi wa watu 1,200 waliouawa na 251 waliotekwa nyara huko Gaza walikuwa raia.

Mauaji na uharibifu huo umesababisha kulaaniwa kwa watu wengi.

[ad_2]

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *