Mwana mkubwa wa kiume wa Rais Donald Trump wa Marekani na ujumbe alioandamana nao wiki iliyopita walikutana na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan mjini Istanbul wiki katika ziara ambayo haikutangazwa. Hayo yameripotiwa na duru zilizodai kuwa na uelewa wa suala hilo.

Taarifa kuhusu ziara hiyo zilifichuliwa kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano na Ozgur Ozel, mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Uturuki cha Republican People’s Party (CHP), ambaye alidai kuwa, Erdogan alikuwa akifanya “mazungumzo ya siri” na mwana mkubwa wa rais wa Marekani Donald Trump Jr kuhusu Ghaza.

“Itifaki ilimtaja kama ‘mfanyabiashara’, lakini hawakutaja jina lake wakati wa ziara,” ameeleza Ozel alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Istanbul na akaongezea kwa kusema: “wakati Palestina inavuja damu, wanafanya biashara na mwana wa Trump kupitia makampuni yenye ushawishi”.

Kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini Uturuki cha CHP amemshutumu rais wa nchi akisema: “kuhusu suala la Palestina, Erdogan anajifanya kumkosoa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, lakini hasemi neno lolote dhidi ya mlezi halisi wa suala hilo, Trump”.

Hata hivyo duru moja ya habari ya Uturuki iliyoko karibu na Erdogan imekanusha madai ya Ozel na kudai kwamba, ni kweli Trump Jr alikutana na rais huyo lakini “alimtembelea kiheshima” tu. Chanzo hicho kimeeleza kwamba, hakukuwa na majadiliano rasmi yaliyofanywa kuhusu Ghaza au mada yoyote maalumu.

Japokuwa Trump Jr hana cheo rasmi katika utawala wa baba yake, lakini anaonekana kuwa na ushawishi mkubwa katika Ikulu ya White House. Kwa sasa anahudumu kama makamu wa rais mtendaji wa Shirika la Trump…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *