
Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Majeshi ya Yemen wametahadharisha kuwa nchi hiyo ya Kiarabu ina uwezo na na njia za kutoa vipigo vikai na kuumiza sana kwa adui Mzayuni iwapo atathubutu kutenda kosa lolote.
“Maadui hasa utawala mtendaji jinai wa Kizayuni, waungaji wake mkono na wanaotetea kiburi cha utawala huo wanapasa kufahamu kuwa tumeboresha jeshi lenye nguvu na kisasa ambalo lina uwezo wa kuilinda Yemen na kuyahami matukufu ya Ulimwengu wa Kiislamu,” wamebainisha Meja Jenerali Mohammed Nassir al Atifi na Muhammad Abdul Karim al Ghamari katika taarifa yao ya pamoja.
Taraifa hiyo ya pamoja imeongeza kuwa vikosi vya ulinzi vya Yemen kwa kutegemea zana za kijeshi zilizoundwa nchini na uwezo wao wa kiulinzi vitatoa mjibizo mkali na wa maumivu makali kwa uchokozi wowote dhidi ya Yemen.
Adui Mzayuni anapasa kufahamu kuwa kitendo chochote cha kunajisi matukufu ya mataifa ya Kiislamu hakitapita bila jibu, Mjibu yetu kwa wavamizi yatakuwa ya kukandamiza na watagharimika pakubwa. imebainisha zaidi taarifa hiyo ya pamoja.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Meja Jenerali Mohammed Nassir al Atifi na Muhammad Abdul Karim al Ghamari Waziri wa Ulinzi wa Yemen na Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo imeisisitiza kuwa utawala ghasibu wa Tel Aviv umetenda jinai isiyosameheka kwa kuishambulia Yemen, na kwamba Israel itakabiliwa na taathira hasi kwa kitendo chake hicho; ikiashiria mashambulizi ya anga ya utawala huo huko Sana’a mji mkuu wa Yemen ya tarehe 28 Agosti yaliyowauwa Ahmed Ghalib al Rahawi Waziri Mkuu wa Yemen na mawaziri kadhaa wa nchi hiyo.