Israel imefanya mashambulizi zaidi katika Ukanda wa Gaza, na kuwaua shahidi Wapalestina wengine kadhaa huku jamii ya kimataifa ikishindwa kukomesha mauaji ya kimbari yautawala huo yanayoungwa mkono na Marekani.

Duru za kitiba zimearifu kuwa, Wapalestina 22 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na utawala wa Israel tangu leo alfajiri. 

Ripoti za awali zimebainisha kuwa wahanga wanne wa jinai ya leo ya utawala wa Kizayuni wameuawa shahidi katika mashambulizi ya anga ya utawala huo yaliyolilenga jengo la makazi ya raia katika mtaa wa Omar al Mukhtar katika mji mkongwe wa Gaza. Wapalestina wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Israel ya leo alfajiri. 

Wapalestina wengine wakiwemo watoto 3 wameuawa shahidi katika hujuma ya leo ya Israel katika kambi ya wakimbizi ya al Shati magharibi wa mji wa Gaza. 

Wakati huo huo, mwanamke mmoja Mpalestina ameuliwa shahidi na wengine watano wamejeruhiwa katika shambulio la Israel katika kambi ya wakimbizi ya al Bureij. 

Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni pia wamewafyatulia risasi na kuwauwa shiahidi wavuvi wawili katika pwani ya mji wa Khan Yunis. 

Wapalestina zaidi ya 65,344 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wadogo wameuawa shahidi tangu Israel ianzishe vita na mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza Oktoba 7, 2023. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *