
Watu zaidi na zaidi wanajiunga na vuguvugu la maandamano yanayotikisa mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo. Licha ya tangazo la Andry Rajoelina siku ya Jumatatu, Septemba 29, la kufutwa kwa serikali nzima, maelfu ya waandamanaji waliendelea kumtaka rais wa Madagascar ajiuzulu siku ya Jumanne, Septemba 30, wakiandamana hadi wilaya ya kati ya mji mkuu ambao hawakuwahi kufikia tangu maandamano yalipoanza Septemba 25.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu huko Antananarivo, Sarah Tétaud
Vuguvugu la vijana Generation Z (Gen Z), ambao wamekuwa wakiongoza kuandaa maandamano nchini Madagascar tangu mwanzo, walikuwa wamepanga waandamanaji wakutane saa 5:00 karibu na Mbuga ya Ambohijatovo, iliyoko chini kabisa ya bonde. Baada ya masaa marefu ya wakikabiliana na vikosi vya usalama katika vitongoji mbalimbali vya mji mkuu, hatimaye waandamanaji waliruhusiwa kwenda Ambohijatovo, wakiimba “Miala Rajoelina” (“Rajoelina, achia ngazi”). Jumbe hizi sasa zilizidi suala la kukatika mara kwa mara kwa maji na umeme.
Karibu saa 9:30 alaasiri, kwa mara ya kwanza kabisa, umati mkubwa wa watu, kutoka vitongoji mbalimbali na miji ya jirani, ulikusanyika mahali hapo. Kulishuhudiwa maandamabo makubwa. Maelfu ya waandamanaji walivamia eneo lililo karibu na bustani hiyo kabla ya polisi, pia kwa wingi na kuungwa mkono na magari ya kivita, kuanza mashambulizi yao ya muda mrefu kwa mabomu ya machozi. Vijana walijilinda, wakirusha mabomu nyuma kwa vikosi vya kuingilia kati kadri walivyoweza. Makabilino haya makali, yanayofanana na vita vya msituni mijini, yaliendelea hadi saa 12:30 jioni.
Siku ya Jumanne jioni, vuguvugu kadhaa za vyama vya wafanyakazi na matawi ya kitaaluma yameeleza kuunga mkono waandamanaji hao, kwa kuanzia na chama cha wafanyakazi wa Jirama, shirika la kitaifa la maji na umeme, amabcho kilitangaza mgomo mkubwa. Chama cha Wanasheria kwa upande wake kilishutumu ukiukwaji mkubwa na unaorudiwa wa haki za binadamu na haki ya kujitetea na kuzitaka mamlaka kufuata Katiba na sheria zinazotumika.
Antananarivo haikuwa jiji pekee kuwahi kushuhudia maandamano. Kaskazini, huko Diego Suarez, maandamano pia yalianza tena siku ya Jumanne kwa madai mapya, sawa na huko Antananarivo: waandamanaji wakitaka Rais Rajoelina kujiuzulu.