Khalid Qaddoumi Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano yaKiislamu ya Palestina Hamas nchini Iran amesema kuwa harakati hiyo ya muqawama ya Palestina imekuwa tayari tangu awali kubadilishana mateka na kusimamisha vita katika Ukanda wa Gaza lakini uvamizi wa kijeshi unaoendelea kufanywa na Israel umezuia kupatikana amani.

“Mpira upo katika uwanja wa Marekani na Israel,” amesema Qaddoumi katika mahojiano maalumu na shirika la habari la IRNA. 

Ameongeza kuwa, msimamo Hamas umejikita katika dhamira yake ya kuhitimisha umwagaji damu unaoendelea kufanywa na Israel na kuwahami wakazi wa Gaza. 

Alipoulizwa katika mahojiano hayo kuhusu msimamo wa Hamas mkabala wa mapendekezo yaliyotolewa na Rais Donald Trump wa Marekani ili kuhitimisha vita vya mauaji ya kimbari huko Gaza, Mwakilishi huyo wa Hamas nchini Iran amebainisha kuwa: “Kama unavyojua, harakati ya muqawama wa Palestina Hamas imepasisha mpango huo kwa masharti  lengo likiwa ni kusimamisha vita na jinai ambazo bado zinaendelea dhidi ya watu wetu huko Gaza, na kuwaondoa wanajeshi vamizi wa Israel na kuwezesha kutumwa misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza.

Amebainisha kusema kuwa, “kwa maneno mengine ni kwamba tulikubali pendekezo la Trump kwa sababu na kwa nia njema.Tutaingia kwenye mazungumzo ili kuhakiki yale ambayo yanapaswa kutekelezwa kwa manufaa ya watu wetu na kukomesha umwagaji damu na jinai za utawala wa Kizayuni, ” amesema Khalid Qaddoumi.

Mwakilishi wa Harakati ya Mapambano yaKiislamu ya Palestina Hamas nchini Iran amesema hali ya mambo ingali inatisha; tangu asubuhi ya leo idadi ya mashahidi imeongezeka huku utawala wa Kizayuni ukiendelea na mashambulizi yake ya anga na ardhini.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *