
Huduma za bima ni nyenzo muhimu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi, zikiwa na mchango mkubwa katika kulinda maisha ya wananchi, mali zao na hata shughuli za kiuchumi.
Huduma za bima hutoa kinga dhidi ya hasara zinazoweza kutokea ghafla, ikiwemo ajali, magonjwa, majanga ya asili au uharibifu wa mali. Kupitia bima ya afya, wananchi hupata huduma bora za matibabu bila mzigo mkubwa wa kifedha. Vilevile, bima ya kilimo na mifugo huwalinda wakulima na wafugaji dhidi ya majanga kama ukame, mafuriko au magonjwa ya mifugo.
Hata hivyo, hapa nchini kiwango cha wananchi kutumia huduma za bima (insurance penetration) bado kipo chini, jambo linalochelewesha ukuaji wa sekta hii na kupunguza mchango wake katika maendeleo ya Taifa.
Ufikishaji wa huduma za bima kwa wananchi wengi zaidi huongeza uhakika wa kifedha na kuhimiza watu kushiriki katika shughuli za kibiashara. Wawekezaji wanapokuwa na uhakika wa kulindwa dhidi ya hasara, hujihusisha zaidi na uwekezaji katika kilimo, viwanda vya uzalishaji, biashara ndogo na kubwa.
Hatua hii pia husaidia serikali kuongeza mapato kupitia kodi kutokana na ukuaji wa sekta mbalimbali. Huduma za bima zinapofikishwa kwa wananchi wengi, zinasaidia familia kuepuka kuanguka kwenye umaskini pindi wanapokumbwa na misukosuko.
Hii inaleta usawa wa kijamii na kuhakikisha watu wote wanapata nafasi ya kujikwamua kimaisha bila kuathiriwa na hatari zisizotarajiwa. Ufikishaji wa huduma za bima kwa wananchi ni chachu ya maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi. Ni wajibu wa Serikali, wadau wa sekta ya bima na taasisi za kifedha kushirikiana kuhakikisha elimu ya bima inawafikia wananchi, huduma zinaboreshwa na gharama zinapunguzwa ili kuwajumuisha watu wengi zaidi.
Strategis Insurance yapiga hodi jijini Mbeya
Ni kwa sababu hii, Kampuni ya bima ya Strategis Insurance imezindua kituo kipya cha mauzo mjini Mbeya, hatua inayolenga kuleta huduma za bima karibu na wateja wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na kuimarisha uwepo wa kampuni katika maeneo muhimu ya Tanzania.
Ufunguzi huu unaashiria mpango wa kimkakati wa kampuni hiyo kuongeza usambazaji wa bidhaa zake, kuboresha upatikanaji wa huduma na kukuza uelewa wa bima miongoni mwa jamii za mikoa ya nyuma ya nchi. Pamoja na mambo mengi ufunguzi wa kituo hicho kitakuwa na faida zifuataoz;
Ufikishaji wa huduma karibu na wateja: Kituo cha mauzo Mbeya kitawafanya wateja wa eneo hilo kupata bidhaa za bima (bima ya afya, bima ya mali, bima ya biashara, bima ya magari, na bidhaa maalum za kilimo) kwa urahisi bila kusafiri umbali mrefu kwenda miji mikubwa.
Ajira na kukuza uchumi: Ufunguzi wa kituo hicho kitasaidia kuzalisha nafasi za ajira za moja kwa moja (wataalamu wa mauzo, huduma kwa wateja) na zisizo za moja kwa moja kama vile mawakala wa bima.
Kukuza uelewa wa bima: Kupitia utoaji wa elimu ya bima, Strategis Insurance itaweza kuongeza idadi ya watu wanaojua na kunufaika na bima, ikisaidia usalama wa kifedha wa kaya na biashara ndogo na za kati (SME’s).
Ufunguzi wa kituo cha mauzo cha Strategis Insurance mjini Mbeya ni hatua ya kimkakati itakayochangia kuongeza upatikanaji wa huduma za bima, kukuza usalama wa kifedha kwa jamii, na kuweka msingi wa upanuzi wa huduma katika mikoa mingine ya Tanzania.
Kwa kutumia mtandao wa mawakala, teknolojia za malipo na kampeni za elimu kwa jamii, kampuni hiyi itaongeza ufikiaji wa huduma za bima na kuleta manufaa kwa wateja, wafanyakazi na uchumi.