Marekani. Mwanamuziki wa Marekani Bradley Younger, maarufu BVB on the Keys ameweka rekodi katika ulimwengu wa muziki kwa kuachia wimbo mpya kila wiki kwa takribani miaka mitatu mfululizo.

BVB amekuwa akitoa wimbo mpya kila wiki bila kukosa kwa zaidi ya miaka miwili na nusu mfululizo, safari aliyoanza mwaka 2022. Huku akihusika kwenye kazi zake zote katika kuandika mistari na kurekodi.

Wengi walidhani msanii huyo angeishia kati lakini alichukua jukumu hilo mpaka mwaka huu 2025 jina lake lilipoingia rasmi kwenye Guinness World Records akiwa pamoja na rafiki yake wa karibu, Dillan Ponders. 

Aidha kupitia mahojiano yake mbalimbali aliyowahi kuyafanya ameweka wazi siri ya mafanikio hayo kuwa ni kujituma kila siku bila visingizio. Huku mara kadhaa akiandika katika ukurasa wake wa Instagram “Kila wiki tunaendelea kuvunja rekodi yetu wenyewe,” akimaanisha kila wimbo anautoa ni hatua mpya katika historia yake.

Hata hivyo, msanii huyo bado anaendelea na utaratibu huku mashabiki wakimtaja kama mashine ya muziki, kutokana na kasi yake ambayo imekuwa ikiwashangaza mastaa wakubwa wanaotamba katika tasnia.

Rekodi hiyo imemshida msanii utoka Sweden, Jens Lekman ambaye aliwahi kutoa nyimbo mpya kila wiki kwa mwaka mzima bila kukosa.

Mpaka sasa, Bradley Younger hajapata tuzo nyingi za muziki za kimataifa. Lakini amepata heshima kubwa kupitia mafanikio yake ya kipekee. Tuzo kubwa zaidi aliyopewa ni rekodi ya dunia kutoka Guinness World Records, aliyoshinda pamoja na msanii mwenzake DillanPonders. 

Msanii huyo anatambulika kupitia ngoma zake mbalimbali ikiwemo C-Notes (with BIGBABYGUCCI), Bionic Man (with DillanPonders), On Me (with BIGBABYGUCCI), Glass House (BVB & Roger Marsil), THIS IS NOT A RAP SONG (BVB Remix), nyimbo ambazo zinazungumzia maisha ya kila siku, mapenzi, changamoto za kijamii, fedha, mafanikio, na maisha ya usanii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *