
Rais aliye madarakani Paul Biya amechaguliwa tena kwa muhula wa nane kwa asilimia 53.66 ya kura, Baraza la Katiba limetangaza siku ya Jumatatu, Oktoba 27. Matokeo ya uchaguzi huo, yaliyofanyika Oktoba 12, yametolewa siku moja baada ya maandamano na mvutano, baada ya waziri wa zamani Issa Tchiroma Bakary kudai ushindi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na Baraza la Katiba na takwimu rasmi zilizotangazwa siku ya Jumatatu, Oktoba 27, mkuu huyo wa nchi anaye maliza muda wake, kutoka Chama cha Cameroon People’s Democratic Movement (CPDM), amechaguliwa tena kwa muhula wa miaka saba, akishinda kwa asilimia 53.66 ya kura, kwa zaidi ya kura milioni 2.47. Baada ya kuiongoza Cameroon kwa miaka 43, Paul Biya, mwenye umri wa miaka 92, sasa anaanza muhula wake wa nane.
Mpinzani mkuu wa Paul Biya, Issa Tchiroma Bakary wa chama cha Cameroon National Salvation Front (CNSF), ambaye alidai ushindi siku moja baada ya uchaguzi na kuwataka wafuasi wake kuandamana siku ya Jumapili, amepata 35.19% ya kura, kwa zaidi ya kura milioni 1.622, kulingana na takwimu kutoka taasisi hiyo. Wakati wa maandamano ya Jumapili huko Douala, mji mkuu wa kiuchumi, watu wanne walifariki, kulingana na mamlaka. Siku ya Jumatatu Oktoba 27 kiongozi wa upinzani amelaani “wizi wa kura” na kulihakikishia shirika la habari la AFP kwamba “tumeshinda bila shaka.”
Cabral Libii ameshika nafasi ya tatu kwa 3.41%, akifuatiwa na Bello Bouba Maïgari kwa 2.45%, na Hermine Patricia Tomaïno Ndam Njoya kwa 1.66%.
Katika kikao cha kutangazwa kwa matokeo, ambacho hakikuhusisha wawakilishi kutoka balozi za nchi za Ulaya na Marekani, Baraza la Katiba limetangaza kwamba kiwango cha ushiriki kilifikia 57.76%. Takwimu rasmi zinaonyesha Issa Tchiroma Bakary akiongoza katika jimbo la Adamawa, jimbo la Kaskazini, na Jimbo la Littoral. Rais Paul Biya, kwa upande wake, amepata ushindi mkubwa, kulingana na taasisi hiyo, kusini (zaidi kwa 90% ya kura), kaskazini magharibi (86.31%), na mashariki (73%).
Matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Cameroon kutoka jimbo kwa jimbo, kulingana na matokeo rasmi
Adamaoua: CPDM: 34.61% / SFNC: 50.33%
Kituo: Kujizuia kupiga kura: 30.15% / CPDM: 70.14% / SFNC: 21.62%
Mashariki: Kujizuia kupiga kura: 33.23% / CPDM: 73.88% / SFNC: 19.82%
Kaskazini ya Mbali: Kujizuia kupiga kura: 41.77% / CPDM: 45.93% / SFNC: 42.34%
Littoral: Kujizuia kupiga kura: 50.64% / CPDM: 20.99% / SFNC: 64.59%
Kaskazini: Kujizuia kupiga kura: 48.47% / CPDM: 38.78% / FSNC: 43.51%
Kaskazini Magharibi: Kujizuia kupiga kura: 52.57% / CPDM: 86.31% / FSNC: 5.21%
Magharibi: Kujizuia kupiga kura: 39.72% / CPDM: 38.61% / FSNC: 46.76%
Kusini: Kujizuaia kupiga kura: 11.72% / CPDM: 90.86% / FSNC: 0.6%
Kusini Magharibi: CPDM: 68.89% / FSNC: 22.79%