Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, imetoa jumla ya shilingi milioni 400 kutoka kwenye makusanyo ya ndani kwa ajili ya mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jumatatu Oktoba 27, 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Juma Hokororo, amesema wanawake wamepata milioni 160, vijana milioni 160, na wenye ulemavu milioni 80.
Hokororo amewahimiza wananchi kuendelea kuomba mikopo na walionufaika kurejesha kwa wakati.
âMwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates