Tabia za Jude Bellingham zimeanza kuchunguzwa upya baada ya nyota huyo wa Real Madrid kuonekana amemdhihaki Lamine Yamal wa Barcelona katika ujumbe wa Instagram baada ya mechi baina ya timu zao ‘El Clasico’.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye alifunga bao la ushindi katika ushindi wa mabao 2-1 wa Real Madrid kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, alichapisha picha yake akisherehekea huku akiwa amenyoosha mikono, iliyonukuu: ‘Kuzungumza ni rahisi. Hala Madrid siempre.’
Ujumbe huo umetafsiriwa na wengi kama jibu kwa Yamal (18) ambaye alizua mvutano kabla ya mchezo kwa kuishutumu Madrid kwa ‘kuiba na kulalamika’.
Hilo linatokea huku kukiwa na hali ya wasiwasi kwa Bellingham juu ya hatima yake katika timu ya taifa.
Kiungo huyo aliachwa nje ya kikosi cha Thomas Tuchel cha timu ya Taifa ya England mapema mwezi huu, huku kocha mkuu akionya kwamba ‘viwango vya maadili haviwezi kujadiliwa’ alipoulizwa kuhusu kutokuwepo kwake.
Tuchel amesema atazungumza na Bellingham kabla ya kuamua iwapo atamuita tena kwa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia mwezi ujao.
Bellingham, ambaye hakucheza wiki kadhaa mapema msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa bega, ameachwa nje ya timu ya taifa hivi karibuni huku Tuchel akijenga kikosi anachosema ‘kinategemea roho, mshikamano na mtazamo sahihi’.
Familia ya nyota huyo wa Uingereza pia imekuwa katika mjadala katika miezi ya hivi karibuni.
Baba yake Mark, ambaye anafanya kazi kama wakala wa Jude na kaka mdogo Jobe, amekuwa akitoa kauli zinazoonekana sio nzuri.
Hivi majuzi aliripotiwa kugombana na maafisa wa Borussia Dortmund akilalamikia muda mchache wa kucheza wa mtoto wake Jude ambaye ni Jobe Bellingham.
Hata hivyo kiwango cha uwanjani na ushawishi wa Bellingham vinaonekana kutokuwa na mashaka.
Pasi yake ya mwisho kwa Kylian Mbappe na bao la ushindi dhidi ya Barcelona viliipa Real Madrid ushindi wa kwanza baada ya kupoteza mechi nne mfululizo za EL Clasico katika na kuifanya iendelee kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Hispania kwa tofauti ya pointi tano.