Kutokana na hali ya ulemavu baada ya kupooza mwili miaka 30 iliyopita, Festo Lusasi mkazi wa Mwangata mkoani Iringa, hatoweza kushiriki uchaguzi wa mwaka huu baada ya kushindwa kujiandikisha.

Lusasi anayewakilisha watu wengine wenye hali kama yake, anasema angependa kuwa mmoja wa wapiga kura. Matamanio yake ni kuona siku zijazo kunawekwa utaratibu wa kuwawezesha watu wenye ulemavu wa aina yake, wenye sifa zinazostahili, kushiriki kikamilifu katika uchaguzi na kutimiza haki hiyo ya kikatiba.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *