Mhifadhi mstaafu wa Makumbusho ya Dk. David Livingstone, Mzee Kassim Mbingo, amewakumbusha Watanzania kujifunza kutoka kwa athari za vita katika nchi jirani za Congo na Burundi, akisema machafuko ya kisiasa katika mataifa hayo ni darasa muhimu kwa Tanzania kuelekea uchaguzi wa Oktoba 2025.
Ametoa wito kwa wananchi kujijengea utamaduni wa amani, kujitokeza kupiga kura kwa wingi, na kuepuka maneno au vitendo vinavyoweza kuchochea vurugu, akisisitiza kuwa amani ni msingi wa maendeleo na urithi wa kizazi kijacho.
✍ Jacob Ruvilo
#AzamTVUpdates