Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dadi Kolimba, ameongoza wananchi katika zoezi la upandaji miti ya mikoko lililofanyika eneo la Sahare kijijini, likiwa na lengo la kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kolimba, ambaye pia alishiriki moja kwa moja katika upandaji huo, amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira na kutambua kuwa uhifadhi wa mikoko ni ngao muhimu dhidi ya mmomonyoko wa ardhi na ongezeko la joto.

Amesisitiza kuwa jitihada za pamoja za wananchi na serikali ndizo zitakazosaidia kulinda mazingira na kuboresha maisha ya jamii za pwani.

✍ Mariam Shedafa
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *