
Divine Makanda, mateka wa kike aliyekuwa anashikiliwa na waasi wa Mobondo katika eneo la Kwamouth, kwenye Wilaya ya Mai-Ndombe nchini DRC ameachiwa huru hapo jana Jumapili ikiwa imepita miezi sita baada ya kutekwa kwake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kuachiwa kwake kulijiri baada ya oparesheni iliyoongozwa na wanajeshi wa DRC (FARDC) kwa ushirikiano na wakaazi kutoka kwenye eneo husika.
Kwa mujibu wa Kapteni Antony Mualushayi, msemaji wa oparesheni Ngemba, Divine Makanda alitekwa tarehe 26 ya mwezi Agosti mwaka huu.
Aidha Mwalushayi amethibitisha kukamatwa kwa wapiganaji wawili kutoka kundi la waasi wa Mobondo wakati wa oparesheni hiyo.
Wakaazi kutoka katika maeneo mengine yenye utovu wa usalama wametakiwa kushirikiana na wanajeshi katika vita dhidi ya utovu wa usalama imesema ripoti ya mtandao wa Radio Okapi.