Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) limeendelea kutoa elimu kwa wadau wa kilimo cha korosho kuhusu matumizi ya mfumo wa mauzo ya minada kwa njia ya kidijitali, ikiwa ni maandalizi ya msimu wa 2025/2026.
Akizungumza mkoani Lindi, Afisa Mwandamizi wa TMX, Justa Martine amesema mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa wa mfumo huo na kuhakikisha uwazi katika biashara. Aidha, aliwataka waendeshaji wa maghala kuzingatia viwango vya ubora vilivyowekwa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) katika upangaji wa korosho.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
