
Kiongozi wa Wakatalani wanaotaka kujitenga, nchini Uhispania, Carles Puigdemont ametangaza siku ya Jumatatu, Oktoba 27, kwamba uongozi wa chama chake umeamua “kusitisha” makubaliano yake na Chama cha Wafanyakazi wa Kisoshalisti nchini Uhispania, ambacho kilimruhusu Pedro Sánchez kuteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu miaka miwili iliyopita.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kiongozi wa Wacatalani wanaotaka kujitenga Carles Puigdemont ametangaza siku ya Jumatatu, Oktoba 27, kwamba uongozi wa chama chake umeamua “kuvunja” makubaliano yake na chama tawala cha Kisoshalisti huko Madrid na kuacha kuunga mkono serikali ya Pedro Sanchez, ambayo haina wingi wa viti katika Bunge.
“Mradi wetu wa kisiasa haulengi utulivu wa Uhispania,” ametangaza Bw. Puigdemont, ambaye anaendelea kuishi uhamishoni nje ya nchi kwa kukwepa mahakama ya Uhispania, wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Perpignan (Pyrénées-Orientales) baada ya mkutano wa chama chake, Junts.
Mgawanyiko huu unaonyesha kuongezeka kwa kutoridhika kwa Junts per Catalunya (JxCat) na serikali ya Pedro Sanchez, ambapo chama cha kinachotetea uhuru wa Catalonia kinaishutumu kwa kushindwa kutimiza ahadi zake.
Hapo awali aliorodhesha malalamiko yake kuhusu kutengwa kwake na Wasoshalisti katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, tangu kuhitimishwa mnamo mwezi Novemba 2023 kwa makubaliano ya usaidizi ambapo wabunge saba wa Junts katika Bunge walimpigia kura Bw. Sanchez ili aweze kurudishwa madarakani.
“Hatuko tayari kuendelea kuunga mkono serikali ambayo haiisaidii Catalonia,” ametangaza. “Ndiyo maana uongozi mkuu katika ngazi ya taifa umeamua kusitisha uungaji mkono wake kwa Chama cha Kisoshalisti, kuingia katika upinzani na, bila shaka, kushauriana na wanaharakati wa chama,” amesema. Amebainisha kuwa mashauriano haya, ambayo yataanza Jumatano saa 4:00 asubuhi na kumalizika Alhamisi saa 12 jioni.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari huko Perpignan (kusini mwa Ufaransa) baada ya mkutano wa chama chake, Junts per Catalunya (JxCat), Carles Puigdemont ameongeza kuwa uamuzi huo “bila shaka” utawasilishwa kwa wanachama wa chama. Hata hivyo, idhini yao haina shaka.