
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa wa kina uhusiano wa kihistoria na mzuri uliopo kati ya Iran na China na kusema: “Uhusiano wa nchi hizo mbili una wigo wa kistratejia na wenye mizizi mirefu.”
Dkt. Ali Akbar Velayati, mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hayo alipokutanba na kufanya mazungumzo na Zhong Peiwu, balozi wa China mjini Tehran ambapo sambamba na kusisitiza juu ya kukita mizizi uhusiano wa kihistoria na mzuri uliopo kati ya Iran na China amesema: “Uhusiano wa nchi hizo mbili una wigo wa kistratejia na wenye mizizi mirefu.”
Katika mazungumzo hayo pande hizo mbili zilisisitiza kuimarishwa na kupanuliwa uhusiano wa kistratijia kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na China na kubadilishana mawazo kuhusu mmatukio ya kieneo na kimataifa. Pande hizo pia zilijadili uhusiano wa pande mbili, matukio ya kimataifa na kieneo, hususan sera za kujitanua za Marekani na uingiliaji wake katika masuala ya ndani ya sehemu mbalimbali za dunia.
Vile vile wamezungumzia uungaji mkono wa Washington kwa jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza. Katika kikao hicho, Velayati ameashiria wa uhusiano mkongwe, wa kihistoria na mzuri kati ya Iran na China na kuesema: “Uhusiano kati ya nchi hizo mbili una mwelekeo wa kistratejia na uliokita mizizi, na ushirikiano kati yao unaweza kupanuka zaidi katika kivuli cha matukio ya kieneo na kimataifa.