Bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Mkuu, mali ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mkuu, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Oktoba 28 mwaka huu.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro, Jeremia Mkomagi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa askari wa zimamoto walifika kwa wakati na kufanikiwa kuuzima moto huo kabla haujasambaa zaidi.

Kwa mujibu wa Kamanda Mkomagi, chanzo cha moto bado hakijajulikana, na uchunguzi unaendelea kubaini sababu halisi ya tukio hilo.

Aidha, amethibitisha kuwa hakuna majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa, ingawa moto huo umeharibu mali kadhaa ikiwemo bweni moja, vitanda 89, magodoro 160, ofisi moja na madaftari ya wanafunzi.

✍ Enoss Masanja
Mhariri @claud_jm
#AzamTvUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *